Friday 27 June 2014

Mr Hongo Song Lyrics

Chorus

Ni kwa nini wanishika afande
na kosa sijafanya
Unasema nimelewa
Na bila hongo ndani nitaenda*2

Ni saubuhi na mapema
Nimeamka nimechangamka tena
Ninapiga magoti namsifu maulana
kwa kunipa siku njema
kisha baadaye kiamsha kinywa
nikimaliza mama kwaheri
tutaonana jioni mola akipendaaa
nashika njia niende stendi nikapande matatu
kwenye barabara napata askari watatu
wananiuliza maswali tena matatu uuu
eti umetoka wapi na unaenda wapi
ebu leta begi kwani umebeba nini
before nijitetee nina pingu mkononi
hongo wanadai nimefanya kosa gani

Chorus

Verse 2
Wakaniweka kwa gari lao
huku mie nimechoka bishana nao
ni serikali aina gani ambayo yadhulumu hadharani
tumejazana ndani ya gari
hapakule ni vijana pia wazazi
wameketi kunyenyekea wengi wao bila kosa kusingiziwa eti


Bridge

Toa hongo ushuke
huu ndio mtindo
haijalishi hata kama hujafanya kosa
tuko kazi mwananchi wewe,wewe*2

Chorus

Verse 3

Huyu mia mwingine thao
wakashuka nikabaki na makarao
haijalishi nitaenda nao
mimi naamini haki itakua ngao yeah!
Tukazidi mdogomdogo hukubado wananiitisha kitu kidogo
Utumishi kwa wote sa imekuwa utoanishi kwa wote
ndio mnone si' tukonde m'dosike si' tusote
haiwezekani!
change inaanza na mimi
lazima nitaibring ata kama ita mean i remain cuffed in these chains sibanduki
I am in the game corruption piga nduki yeah!

Chorus

Get whole album here and download it for freehttp://noisetrade.com/jayplusinternational/raindrops

No comments:

Post a Comment